Monday, May 22, 2017

MWENGE WA UHURU 2017 WAPOKELEWA MKOANI LINDI NA KUKIMBIZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA LINDI

Wakulima Wilayani Lindi wameaswa kushiriki utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya 5 Katika kufikia na kufanikiwa kuwa  nchi yenye uchumi wa viwanda. Wito huo umetolewa leo kijijini Kiwalala, na mmoja wa wakikimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa, Frederick Ndahani, alipozungumza na wananchi kwa niaba ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa. Ndahani alisema wakulima wanawajibu wa kushiriki kikamilifu wa kuifanya nchi kuwa na uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.
Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wananchi wanaoishi wilayani humo ni wakulima, hivyo wana nafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali kupitia kazi wanayofanya. Ndahani alifafanua kuwa ili wakulima waweze kufanisha azima hiyo hawana budi kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye viwanda.
“Badala ya kuuza mazao ghafi wakulima wafikirie kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwakufanya hivyo mtakuwa mmeongeza thamani mazao mnayozalisha,” alisema Ndahani. Aliongeza kuzitaja faida za kuwa na nchi ya viwanda kuwa ni kuongeza ajira ya mtu mmojammoja, kukuza uchumi wa taifa na kutoa fursa zinazo toa ajira. “Lengo nikuona hadi kufikia mwaka 2025 wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini nakufikia uchumi wa kati,” alisisitiza Ndahani.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu ni Ndugu Amour A. Amour akisaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).

Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'

Mwenge wa Uhuru hapa Mkoani Lindi unatarajiwa kuzunguka katika Halmashauri zote 6 kuanzia tarehe 21 - 26 May 2017, ukipita kwenye miradi mbalimbali ya kuwekewa jiwe la msingi, kuonwa, na kuzinduliwa. Leo utakabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na mkesha wa usiku utakuwa katika Uwanja wa Ilulu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 ulizinduliwa rasmi tarehe 2/4/2017 katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi. 
 Pichani juu ni Wakimbiza Mwenge walipokuwa wakivishwa Skafu kama ishara ya kupokelewa katika Wilaya ya Lindi hususani Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.

UHURU TORCH


The Uhuru Torch symbolizes freedom and light. It was first lit on top of Mount Kilimanjaro in 1961. Symbolically to shine the country and across the borders to bring hope where there is despair, love where there is enemity and respect where there is hatred. Yearly there is the Uhuru Torch race, starting from different regions throughout Tanzania, to remind Tanzanians of their duty to jealously guard their cherished freedom, unity and peace.

Wednesday, May 10, 2017

Taratibu za Kupandishwa Vyeo na Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa



Imetolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

1.0 Utangulizi
Usimamizi wa Watumshi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika masuala ya upandishwaji vyeo, mafunzo na uhamisho yameelezwa katika Sheria ya Utumshi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002, ikisomwa pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na Taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na Miongozo na Nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali. Kwa sasa taratibu za kusimamia masuala hayo soma zaidi bonyeza HAPA

Wednesday, May 3, 2017

CHAPISHO LA MAJARIBIO

MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA LINDI NI MWEZI MAY 2017
 Wataalamu na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi wakitoa heshima zao kwa Mwenge wa Uhuru baada ya makabidhiano kutoka Manispaa ya Lindi katika kiwanja cha michezo Mchinga 1 mwaka 2016
 Mbunge wa Mtama Mh. Nape Moses Nnauye akiwahi tukio moja katika mbio za Mwenge mwaka 2016