Wakulima Wilayani
Lindi wameaswa kushiriki utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya 5 Katika
kufikia na kufanikiwa kuwa nchi yenye
uchumi wa viwanda. Wito huo umetolewa leo kijijini Kiwalala, na mmoja wa
wakikimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa, Frederick Ndahani, alipozungumza na wananchi
kwa niaba ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa. Ndahani alisema
wakulima wanawajibu wa kushiriki kikamilifu wa kuifanya nchi kuwa na uchumi wa
viwanda kupitia sekta ya kilimo.
Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wananchi
wanaoishi wilayani humo ni wakulima, hivyo wana nafasi ya kushiriki mpango huo
wa serikali kupitia kazi wanayofanya. Ndahani alifafanua kuwa ili wakulima
waweze kufanisha azima hiyo hawana budi kubadilisha mtazamo na fikra kutoka
kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye viwanda.
“Badala ya kuuza mazao ghafi
wakulima wafikirie kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwakufanya hivyo mtakuwa
mmeongeza thamani mazao mnayozalisha,” alisema Ndahani. Aliongeza kuzitaja faida za kuwa na nchi
ya viwanda kuwa ni kuongeza ajira ya mtu mmojammoja, kukuza uchumi wa taifa na
kutoa fursa zinazo toa ajira. “Lengo nikuona hadi kufikia
mwaka 2025 wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini nakufikia uchumi wa
kati,” alisisitiza
Ndahani.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge mwaka huu ni Ndugu Amour A. Amour akisaidiana na wenzake watano katika
kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi
Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia
Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).
Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI
KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'
Mwenge wa Uhuru hapa Mkoani Lindi unatarajiwa kuzunguka
katika Halmashauri zote 6 kuanzia tarehe 21 - 26 May 2017, ukipita kwenye
miradi mbalimbali ya kuwekewa jiwe la msingi, kuonwa, na kuzinduliwa. Leo utakabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na
mkesha wa usiku utakuwa katika Uwanja wa Ilulu.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa
mwaka 2017 ulizinduliwa rasmi tarehe 2/4/2017 katika
uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi.
Pichani juu ni Wakimbiza Mwenge walipokuwa wakivishwa Skafu kama ishara ya kupokelewa katika Wilaya ya Lindi hususani Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.