Monday, May 22, 2017

MWENGE WA UHURU 2017 WAPOKELEWA MKOANI LINDI NA KUKIMBIZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA LINDI

Wakulima Wilayani Lindi wameaswa kushiriki utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya 5 Katika kufikia na kufanikiwa kuwa  nchi yenye uchumi wa viwanda. Wito huo umetolewa leo kijijini Kiwalala, na mmoja wa wakikimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa, Frederick Ndahani, alipozungumza na wananchi kwa niaba ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa. Ndahani alisema wakulima wanawajibu wa kushiriki kikamilifu wa kuifanya nchi kuwa na uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.
Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wananchi wanaoishi wilayani humo ni wakulima, hivyo wana nafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali kupitia kazi wanayofanya. Ndahani alifafanua kuwa ili wakulima waweze kufanisha azima hiyo hawana budi kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye viwanda.
“Badala ya kuuza mazao ghafi wakulima wafikirie kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwakufanya hivyo mtakuwa mmeongeza thamani mazao mnayozalisha,” alisema Ndahani. Aliongeza kuzitaja faida za kuwa na nchi ya viwanda kuwa ni kuongeza ajira ya mtu mmojammoja, kukuza uchumi wa taifa na kutoa fursa zinazo toa ajira. “Lengo nikuona hadi kufikia mwaka 2025 wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini nakufikia uchumi wa kati,” alisisitiza Ndahani.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu ni Ndugu Amour A. Amour akisaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).

Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'

Mwenge wa Uhuru hapa Mkoani Lindi unatarajiwa kuzunguka katika Halmashauri zote 6 kuanzia tarehe 21 - 26 May 2017, ukipita kwenye miradi mbalimbali ya kuwekewa jiwe la msingi, kuonwa, na kuzinduliwa. Leo utakabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na mkesha wa usiku utakuwa katika Uwanja wa Ilulu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 ulizinduliwa rasmi tarehe 2/4/2017 katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi. 
 Pichani juu ni Wakimbiza Mwenge walipokuwa wakivishwa Skafu kama ishara ya kupokelewa katika Wilaya ya Lindi hususani Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.
PICHA ZINAZOFUATA ni baadhi ya miradi iliyozinduliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.








No comments:

Post a Comment